Semeni amekuwa akijaribu kumuonya Sophia kwa muda sasa. Kama mke mkubwa anajua tabia yake na inaonekana kama baada Iddy kumchoka Sophia alikutana na Judith. Ingawa Semeni ameshamuonya Sophia kwamba Iddy sio muaminifu, kuna ishara mtu anaye cheat amabazo Sophia hataki kuziona kwake. Hapo chini tumekupa orodha ya vitu ambavyo unaweza kuona kama mpenzi wako sio muaminifu:
- Mabadiliko katika Tabia
Ikiwa ghafla mpenzi wako amebadilika tabia bila sababu za wazi, huenda ikawa ishara ya kuwa kuna kitu anachochea. Mwanzoni Iddy alikuwa akimpenda na kumtetea Sophia, siku hizi hataki hata kuonana nae.
- Kutokuwa na Wakati wa Kutosha
Ikiwa mpenzi wako mara nyingi anakuwa na shughuli zisizo za kawaida na hana wakati wa kutosha kuwa nawe, huenda ikawa ni ishara ya kutafuta wakati wa kutosha kwa mtu mwingine. Kila siku Iddy amekuwa akishinda kazini na mitaani kuliko hata nyumbani.
- Simu na Ujumbe wa Siri
Ikiwa mpenzi wako anaficha simu yake au ana tabia ya kupokea simu kwa siri, hii inaweza kuwa ishara ya kuficha mawasiliano na mtu fulani. Vilevile, mabadiliko katika matumizi ya mitandao ya kijamii au kutokuwa tayari kushiriki nywila za akaunti zao kunaweza kuongeza wasiwasi.
- Kupoteza Hamu ya kuonana na wewe
Mtu akikupenda ni lazima apende kuwa karibu na wewe kama mpenzi wake, lakini ukishaona umbali na mabadiliko katika hapo ni lazima uwe na wasiwasi kama bado yupo kwako.
- Kutokuelewana Katika Mazungumzo
Kukwepa mazungumzo au kutoa majibu ya kuepuka kunaweza kuashiria kujaribu kuficha kitu. Tangu Iddy alivyomuona Judith, kila akiongea na Sophia ni kelele na mapigano mengi.
Jiunge nasi kila Jumatato hadi Jumapili saa 3:30 usiku kwa vipindi vipya vya #MMBJuaKali ndani ya DStv chaneli 160 pekee!