Logo
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Zawadi za kumpa Baba yako kwenye sikukuu ya Baba Duniani!

News
16 Juni 2023
Mpe baba yako zawadi atakayoikumbuka!
Article

Tunapoelekea katiks shamrashamra za  siku ya Baba duniani, ni wakati mzuri wa kuonyesha upendo na kushukuru baba zetu kwa mengi waliyotofanyia , na jukumu lake kubwa katika familia. Kwa msaada kutoka kwa wahusika wa Maisha Magic Bongo, tumekusanya orodha za zawadi ambazo unaweza kumpa baba yako.

Kofia 🤠 (Nguzo – Mpali)

Umri ukizidi na nywele zinazidi kupungua kwa wanaume wengi. Chagua kofia kama ya Nguzo ndani ya tamthilia ya #MMBMpali kwa ajili ya baba yako.

Kompyuta Ndogo 💻 (Thomas – Jua Kali)

Kwa baba ambaye anapenda teknolojia, zawadi ya kompyuta ndogo itakuwa nzuri. Kwa mtu kama Thomas wa #MMBJuaKali anavyotuonyesha matumizi husika na kifaa hichi.

Kitabu 📚 (Chifu Pingu - Mwali)

Wengi wetu tunapenda kusoma, na baba zetu pia! Kwa sasa hivi Chifu Pingu wa #MMBMwali anaumwa na muda mwingi yupo ndani na kupitisha muda anasoma kidogo. Kwa baba yako unaweza kuchagua kitabu kinachofaa.

Vifaa vya Michezo 💪 (Roy – Huba)

Baba kama Roy amabaye bado ni kijana anapenda michezo, zawadi kama jezi ya timu anayoipenda, mpira, au kifaa cha kuchezea mchezo atakifurahia.

Je ni zawadi gani unaipenda zaidi? Tuambie hapo chini 👇Pia tunapenda kuwatakia baba zetu  wote kheri ya siku hi maalum kwao.

 

Zawadi ya baba!

Ni zawadi gani ungependa kumpa baba yako kwenye sikukuu ya wakina baba?

Kofia67%
Kompyuta ndogo0%
Vitabu0%
Vifaa vya Michezo33%