Mheshimiwa Pindi Chana, alionekana katika majukwaa mengi akihimiza kukuza Sanaa na vipaji kwa vijana nchini , hili limedhihirika baada yay eye binafsi kuchukua hatua hii ya kujiunga na wadau wake live kabisa , jambo ambalo sio tu limeshangaza wengi bali kuwafurahisha wengi pia kwani sii kitu cha kawaida kwa mheshimiwa kuigiza na ni viongozi wachache sana wamewahi kufanya kama yeye.
Ndani ya kipindi cha #MMBJuaKali Mheshimiwa Pindi anaigiza kama Paulina, ambaye ni mkurugenzi wa wakaguzi wa mashirika ya kutoa msaada katika jamii , yaanii NGO. Na ana anza kazi yake kwa kumuonya Professa kuhusu mambo anayoyafanya.
Kazi kwako mtazamaji , usikose kushuhudia seke seke la mheshimiwa katika Juakali kila Jumatano-Jumapili saa 3:30 Usiku kupitia Maisha Magic Bongo pekee!
Heko nyingi kwako DR Pindi Chana umekuwa kiongozi na mfano wa kuigwa na wengi.