Logo
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Mapenzi ya Lukas: Kukabiliana na Kansa na Kuwa Mwamba kwa Femi – Jua Kali

Habari
20 Novemba 2023
Baada ya Lukas kupata taarifa kwamba Femi anaumwa na kansa ya damu, daktari amhimiza Lukas kujikaza na kuwa mwamba kwa Femi.
Jua Kali

 

Mpenzi wako akipata ugonjwa mgumu kama wa saratani, ni muhimu sana kutoa msaada na upendo wa dhati. Kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kusaidia mpendwa wako kupitia kipindi hiki kigumu. Baada ya kugundua kwamba mke wake yupo karibu na kifo baada ya ugonjwa wake, daktari wa Femi amuhimiza Lukas kuzidi kumtia moyo.

  1. Kuwa na mawasiliano mazuri ni muhimu.

Tangu mwanzo, Lukas hakuwa na mawasiliano mazuri na Femi ndiyo maana kwa muda mrefu Femi alificha ugonjwa wake. Wewe kama mpenzi tafuta muda wa kuzungumza na mpenzi wako kuhusu hisia zake, wasiwasi, na matarajio. Kusikiliza kwa makini kunaweza kutoa faraja na kujenga nguvu ya pamoja.

  1. Kuonyesha upendo na kujali.

Kwa sababu Femi amekuwa ndani ya maumivu anahitaji Lukas kumuonyesha upendo wake wote. Kuwa karibu na mpenzi wako kwa njia ya kimwili na kihisia kunaweza kusaidia kujenga hisia za usalama na faraja.

  1. Kusaidia katika ratiba za matibabu ni hatua nyingine muhimu.

Femi atahitaji matibabu na kwenda kwa daktari mara nyingi, ni viruzi kama mpenzi wake, Lukas kutoa msaada kwa kuhudhuria miadi ya daktari, kutoa usafiri, au kusaidia na kazi za nyumbani kunaweza kupunguza mzigo wa mpenzi wako.

  1. Weka mazingira ya kufurahisha na matumaini.

Daktari alimuomba Lukas awe na matumaini na azidi kumuombea Femi. Kufanya shughuli za pamoja, kama vile kucheka pamoja au kufanya mambo wanayopenda, kunaweza kuwa na athari chanya kwa afya yao ya kimwili na kihisia.

  1.  Kuwa na subira na uelewaji ni muhimu sana.

 Kuelewa kwamba safari ya kupona inaweza kuwa ngumu, na kuonyesha uvumilivu kunaweza kuimarisha uhusiano wenu.

Jua Kali
Femi - Jua Kali

Je unafikiri Femi atapona nah ii kansa ya damu, au ndiyo mwisho wa safari?

Atapona!60%
Mwisho wa safari!40%

Usikose kipindi cha #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku ndani ya #MaishaMagicBongo