Logo
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Jua Kali tunavuka boda!

News
10 Mei 2023
Tamthilia ya Juakali kwa muda sasa imekuwa ikileta vionjo vya tofauti tofauti kwa Watazamaji, tumepata fursa ya kupata vionjo kutoka wkwa wasanii mbali mbali ndani na nje yan chi ikiwemo wasanii kutoka Ghana , Afrika Kusini na Kenya.
Jua Kali

Msimu huu wa 6 umeanza na shamra shamra za msanii Rabby Bray aliejiunga na wana Juakali chini ya Direkta Leah Mwendamseka wa Lamata village Entertainment mwanzoni kabisa wa msimu huu.

Rabby alikuja kuleta mtafaruko katika penzi la Anna na Diba ambapoa Anna anaonekana kutokuwa na msimamo  na hivi sasa anaonekana kurudi Ghana ili kuendeleza stori ya Anna ,Diba Pamoja na Bobo. 
 


Endelea kufuatilia Juakali tugundue yatakayojiri katika hili penzi lenye tashtiti . Hatukuishia hapo tukiendela na simulizi la Juakali , Lamata Village entertainment hivi sasa imeongeza chumvi kwa kugonga hodi katika nchi jiranii Kenya . 
Huku tumemuendea nguli kabisa wa kazi hizi za Sanaa za uigizaji kijana mtanashati Pacal Tokodi almarufu kama ‘Nelson’ aliyetuwaa jina na umaarufun  kupitia telenovela iliyoruka kupita channeli ya nchini humo. Pascal anakuja kwa jina la Tonny katika Juakali , huku anakuja kama aliyekuwa mpenzi wa Femi na rafiki mkubwa wa Frank. 

Ijulikane kwamba Frank na Luka ambaye ndio mpenzi wa sasa wa Femi wana historia chungu zana iliyofanikiwa kutingisha na kusikitisha watazamaji wengi wa tamthilia hii. 
Hadi sasa tumeshuhudia Femi akisimama na msimamo wake na Luka akidhania kwamba ni Frank ndie anae jaribu tena kuingilia mahusiano yake . 

Fuatilia haya na mengine mengi katika #MMBJuakali inayoruka kila Jumatano-Jumapili kupitia MMB Dstv channeli 160 

Je ni nini haswa kitaendela Tonny atakubali kuachana na Femi kirahisi au ndio mpambano wa jua kumuwakia Luka unaanza tena? 👇

 

Jua Kali
Tonny - Jua Kali

Je ni nini haswa kitaendela Tonny atakubali kuachana na Femi kirahisi au ndio mpambano wa jua kumuwakia Luka unaanza tena? 

Tonny ataachana na Femi kirahisi40%
Luka atapambana na Tonny juu ya Femi60%