Logo
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Je Frank au Thomas? - Jua Kali

Habari
17 Novemba 2023
Ujauzito wa Maria ni wa nani?
Jua Kali

 

Mwanakondoo Maria ameyakanyaga , kama tunavyojua Maria amekuwa akiwachanganya Thomas na Frank kwenye mahusiano kwa muda mrefu sasa. Kabla ya kuanzisha mahusiano na kaka Fuleh apo nyuma , alikuwa tayari kwenye mahusiano na Lukas. Baada ya kukutana na Frank alimgeuka na kumsababishia dhuruba kubwa,  wakati huo huo  alikua akimchanganya Thomas na mwanae Felix.

Na kwa sasa Maria na Frank bado hawajaweka mambo yao saw ani baada ya kugundulika kwamba mtoto wa Michael ni wake na Mary kutoweka .

Maria akarudisha majeshi kwa Thomas kwa nguvu zote siku za hivi karibuni na amegundua ana ujauzito na hajui ni wa nani kati ya Thomas au Frank  , amefanya maamuzi ya kuto kuitoa hiyo mimba huku akiwa na mpango wa kuwabebesha majukumu Frank Pamoja na Thomas.

Je atafanikiwa kuwapanga bila ya wao kujua?

Jua Kali
Frank au Thomas? - Jua Kali

Ujauzito wa Maria ni wa nani?

Click here to make your selection
Jua Kali
Frank
Jua Kali
Thomas

Usikose kuangalia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku ndani ya #MaishaMagicBongo