Kuanza, Romy Jons au kama anavyo fahamika ndani ya #JuaKaliTZ kama Bill JR, alijitambulisha na kutaka kujua je ni kundi gani la Frank na ni kundi gani la Bill? Kwasababu Frank na Bill wote wanampenda Naira lakini upendo wa Frank unamtesa Naira wakati Bill hajapata nafasi ya kuwa na Naira na hilo linamuumiza.
La pili Romy Jons alilotaka kujua ni kwani kuna maFrank kwenye maisha yenu? Je kuna mtu ambaye unamjua ambayo kuyu kwenye idara ya juu au bosi lakini anatumia nafasi yake ya nguvu kuwanyanyasa wafanya kazi wake kama Frank anavyomfanya Naira.
Hatimaye Bill aliongelea kuhusu mahusiano yake na Naira, anadai eti anampenda sana lakini ajui afanye nini ili Naira amkubali.
Kama ulikosa live yeyote unaweza kutembelea mtandao wetu wa jamii wa Instagram (@maishamagicbongo) ili uweze kujua kila kitu kinachoendelea ndani ya #JuaKaliTZ.
