Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Patience Ozokwor kurindima ndani ya Jua Kali

Habari
16 Machi 2022
Jua Kali inajumuisha mtaalamu na mshindi wa tuzo, Patience Ozokwor
MMB JuaKaliFeatPatienceSM V1 ShowpageBillboard HR

Ikiwa ni zaidi ya miongo miwili akiwa katika tasnia ya uigizaji, Patience Ozokwor amejitwalia umaarufu mkubwa katika tasnia ya filamu na burudani. Ukitazama neno "kipaji" katika kamusi, bila shaka utapata jina la Patience na vilevile majukumu ya kipekee ambayo amecheza katika maisha yake yote ya uigizaji.

Mshindi wa tuzo na mwigizaji nguli (anayejulikana kwa jina la Mama G) sasa ataonekana kwa mara ya kwanza katika tamthilia ya Jua Kali mnamo Jumatano 16 Machi kama shangazi wa Zozo- Bobo. "Tunafuraha na ni heshima kubwa kufanya kazi pamoja na Patience Ozokwor na tunatarajia mapinduzi makubwa katika tamthilia ya Jua Kali," alisema Barbara Kambogi, Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo.

Patience Ozokwor - Jua Kali

Umeshamuona Patience Ozokwor (Aunty Zozo) ndani ya Jua Kali? Tuambie hapo chini

Ndio67%
Hapana, bado naangalia vipindi vya zamani33%

Kutana na Patience kwenye #MMBJuaKali kuanzia tarehe 16 Machi na kila Jumatano hadi Ijumaa saa 9.30 usiku .Kutokana na maombi ya watazamaji na wapenzi wa tamthilia ya #MMBJuaKali, tamthilia hii itakua ikirushwa mara tano kwa wiki kila Jumatano hadi Jumapili kuanzia tarehe 30 Machi. Ndiyo, maoni yametufikia na tumeyafanyia kazi, usikose kutazama yanayojiri katika tamthilia ya #MMBJuaKali.