channel logo dark
Season 14
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Daktari mpya ndani ya Huba

Habari
29 Julai 2021
Dkt. Nelly amekuja kumsahidia Devi ilia pone miguu, je kuna mpango mwingine aliokuwa nao?
Screenshot 2021 07 28 at 23

Baada ya Devi kupata ajali, kila mtu alishituka. Alikuwa anaenda kusimamisha harusi ya Tima na Jude baada ya kugundua bado ana hisia  kwa Tima.

Ajali ya Devi iliwakasirisha watu wengi kuanzia mama yake na Devi, Tesa harafu mke wake na Devi, Kibibi. Baada ya ajali, Devi alisafirishwa hospitali ambapo walimtia ICU alivyofika. Baada ya kukosa fahamu kwa siku kadhaa, alifanikiwa kuamka.

Kibibi kama mke ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwa karibu na Devi kipindi alivyoaamuka. Lakini baada ya kugundua kwamba Devi alikuwa ana mkimbilia Tima kabla ya ajali yake. Hili jambo lili mkasirisha sana. Kibibi aliamua kujaribu kumuua Devi lakini hakufanikiwa lakini baada ya Devi kupata fahamu waligundua kwamba miguu yake imepooza na kwamba hato weza kutembea tena. Hapo ndipo Devi akapewa mtaalamu mpya, Dk Nelly, ambaye ndiye mtaalamu wa miguu na ameweka afanye kazi na Devi ili amsahidie.

Tatizo kubwa na Dkt. Nelly ni kwamba ni mzuri, mkarimu na ana mpenda sana Devi. Kwa sasa hivi Devi na Kibibi wana matatizo ndani ya ndoa yao. Je wakati Dkt Nelly na Devi wanafanya kazi Pamoja, hisia zinaweza kutokea? Fuatilia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku kugundua.