channel logo dark
Huba
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Nani anaongoza ku-cheat? – Maisha Magic Bongo

Habari
20 Agosti 2024
JB aongeza nyumba ndogo na Anna aanza mahusiano na Devis kazini.
Article

Katika ulimwengu wa mapenzi na ndoa, suala la usaliti limekuwa na sura mbili tofauti. Katika tamthilia maarufu za Maisha Magic Bongo, za Huba na Jua Kali, tunashuhudia visa vya usaliti kutoka pande zote za jinsia.

Kwanza, kuna JB kutoka Huba, ingawa JB ana wake wawili tamaa bado haijaisha. Hivi karibuni JB ameanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nicole. Kuwa nyumba ndogo sio kitu kigeni kwa JB. Kabla ya Nicole, alikuwa na mahusiano ya kisiri na mama wa kambo wa mke wake wa kwanza, Tima. Ingawa mahusiano hayo yalikuwa siri na wake zake Tima na Happy bado hawajui, watazamaji wanajua. Je itakuaje wake zake wakigundua ukweli.

Majini wamfuata JB akiwa na Nicole

Kwa upande mwingine, tunakutana na Anna ndani ya Jua Kali, ambaye amekuwa katika uhusiano mgumu na Diba kabla ya kufunga ndoa. Licha ya kuolewa hivi karibuni, Anna ameanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi mwenzake, Devis, huku akimficha mume wake, Diba. Hii pia sio mara ya kwanza kwa Anna kutembea nje ya mahusiano yake na Diba. Kabla ya Devis, kulikuwa na Bobo, mchumba wa zamani wa Anna. Baada ya Bobo kurudi Tanzania, Anna alianza mahusiano ya kisiri nae wakati bado aliyvokuwa na Diba na ilichua muda kwa Diba kumsamehe na kukubali wafunge ndoa. Je Diba atamfanya nini mara hii akigundua kwamba, tena ana mahusiano ya nje ya ndoa yao?

Anna akutana na Devis

JB anawakilisha wanaume ambao licha ya kuwa na familia wanaendelea kuwa na nyumba ndogo, huku Anna akionyesha kuwa hata wanawake wanaweza kuingia katika usaliti wa kimapenzi. Kwa hivyo, swali la nani anaongoza kucheat kati ya wanawake na wanaume?

Wanaume au wanawake

Kati ya wanawake na wanaume, nani anaongoza ku-cheat?

Huba
Wanaume81%
Jua Kali
Wanawake19%

Usipitwe na hizi tamthilia zinazongoza ndani ya Maisha Magic Bongo, jiunge nasi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku kwa kipindi cha #MMBHuba na kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku kwa kipindi cha #MMBJuaKali kupitia Dstv chaneli 160.