Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Septemba hii ndani ya Maisha Magic Bongo!

Habari
01 Septemba 2023
Baadhi ya vipindi vya kuburudika navyo mwezi huu ndani ya DStv chaneli 160
Article

Huba

Jiunge nasi kwa msimu was 12 wa #MMBHuba, tamthilia inayohusu mapenzi, pesa, ubinafsi na uchawi. Ndani ya mwezi huu gundua kama Tima na JB watafanikiwa kufunga ndoa yao wakati Watoto wa JB wakiwa wanamsumbua. Jiunge nasi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku kwa vipindi vipya.

 

Jua Kali

Mwezi huu tunaendelea na msimu wa sita wa #MMBJuaKali, hii tamthilia inafuatilia Professa Bill ambaye ni bingwa wa hesabu akiwa anatumia watu tofauti na familia yake. Baada ya Stella kurudi na kufunmwa na Felix akiwa na Thomas, je mambo yatakuaje huko mbele? Jiunge nasi kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku kwa vipindi vipya.

 

Divas & Hustlas

Endelea kufuatilia msimu wa kwanza wa #MMBDivasAndHustlas na fuatilia wabunifu kwenye tasnia ya burudani wakiwa wanapambana kukuza brand zao Pamoja na changamoto zote. Jiunge nasi kila Alhamisi saa 1 usiku kwa vipindi vipya.

 

Wimbi

Fuatilia msimu wa kwanza wa #MMBWimbi ukifuatilia wivu, tamaa, mapenzi na migogoro kati ya James na mke wake wakati mama yake James, Biha akiwa katikati yao. Jiunge nasi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku kwa vipindi vipya.

 

Mwali

Mwezi huu tunakuletea msimu wa mwisho wa #MMBMwali, fuatilia penzi kati ya Mwali na Nozo, je waishia pamoja? Jiunge nasi kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku kwa vipindi vipya.

 

Kumbuka kwamba unaweza kufuatilia hivi vipindi vyote kwa njia ya Showmax na DStv Stream popote ulipo.