Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Ingizo jipya ndani ya HUBA Fahyvanny (FEI)! - Maisha Magic Bongo

News
06 Julai 2023
Fahyma maarufu kama Fahyvanny AKA “Mrs Chui” mapema wiki hii amejiunga rasmi na famlia ya Tamthilia ya #MMBHuba
Huba

Tamthilia ya Huba inazidi kuongeza sio tu ubora katika burudani bali ni mmoja ya tamthilia kongwe inayopendwa sana nchini Tanzania. Tamthilia hii inayoruka kupitia channeli ya Dstv Maisha Magic Bongo pia imefanikiwa kujitwalia tuzo mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Mapema wiki hii, Fahyma anajiunga nasi , tofauti na yeye kuwa mama mtoto wa msanii maarufu Rayvanny , Fahyma  amejijengea jina ndani sekta ya burudani na pia kwenye mitandao ya jamii na kwa sasa ameamua kutuonyesha kipaji chake cha uigizaji. Fahyvanny atakuwa akiigiza kama, Fei, mtoto wa Ruby. Anakuja baada ya kifo cha Ruby mama yake Nelly na kudai kwamba yeye pia ni mtoto wa Ruby , anaingia kwa kishindo na tashtiti za kutosha huku sio tu kuwashtua bali anawashangaza kina JB  na Yakub anaonekana kujua zaidi kuhusu stori ya Fei na mama yake Ruby , ili kujua yatakayojiri fuatilia tamthilia ya #MMBHuba , kila Jumatatu-Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Dstv channeli 160!

Kwa zaidi: 

Huba
Fei - Huba

Umeshamuangalia Fei ndani ya #MMBHuba?

Ndiyo98%
Hapana2%