Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Bahati mbaya zinazoweza kutokea ndani ya Harusi ya Nelly na Devi! – Huba

News
31 Mei 2023
Harusi za Devi zinatokea na kasheshe nyingi, je ni bahati mbaya gani itamkumba akimuoa Nelly?
Huba S12


Wakati siku za harusi ni za furaha na shangwe, mambo mabaya yanaweza kutokea na kuharibu kumbukumbu nzuri za siku hiyo muhimu. Bahati mbaya ni suala linaloweza kujitokeza katika harusi yoyote lakini inaoneka kama bahati mbaya inamfuataga Devi sana kwenye siku ya harusi yake. Hapa chini ni mambo matano ya bahati mbaya yanayoweza kutokea katika harusi ya Nelly na Devi

Mvua kunyesha
Mvua kunyesha ni jambo linaloweza kuvuruga mipango yote ya harusi. Kwa mpango Tesa aliofanya kutaarisha hiyo harusi, bahati mbaya inaweza kutokea na mvua ikanyesha. Mvua inaweza kuleta uchafu na matatizo ya usafiri, kuharibu mavazi ya harusi, na kufanya hafla iwe ya kukatisha tamaa kwa wageni na maharusi wenyewe.

Kuchelewa kwa harusi
Ingawa Tesa ang’ang’ania kwamba hataki Uswahili ndani ya harusi ya Nelly na Devi. Lakini katika harusi nyingi, kuchelewa ni jambo linalowezekana. Inaweza kuwa ni kuchelewa kwa wahudumu wa harusi, wapambe au hata maharusi wenyewe. Hii inaweza kusababishwa na sababu zisizotarajiwa kama matatizo ya usafiri au hitilafu zisizotarajiwa. Kuchelewa kunaweza kuvuruga ratiba ya harusi na kuwafanya wageni wawe na wasiwasi na kutokuwa na furaha.

Chakula kutotosha
Ingawa wageni hawatokuwa wengi, bado kuna wasiwasi wa chakula kuchelewa. Chakula ni sehemu muhimu ya harusi na ni muhimu kuwahakikishia wageni chakula cha kutosha na cha ubora. Hata hivyo, kuna wakati mwingine ambapo chakula kinaweza kutosha kwa sababu zisizotarajiwa. Inaweza kuwa ni kwa sababu ya kupungukiwa na idadi ya wageni, matatizo ya kupika, au hitilafu ya usambazaji wa chakula. Hii inaweza kusababisha hasira na kutofurahishwa kwa wageni na kuathiri sifa ya harusi.

Matatizo ya umeme
Nguvu za umeme zinaweza kuwa suala katika harusi nyingi hapa Tanzania. Matatizo ya umeme yanaweza kusababisha kukatika kwa taa za mapambo, muziki, na hata vifaa vingine muhimu. Hii inaweza kusababisha kukatishwa tamaa kwa wageni na kuharibu mazingira ya jumla ya harusi. Ni muhimu kuwa na mpango wa dharura au jenereta ili kukabiliana na matatizo ya umeme yanapotokea. Lakini tuombe Mungu kwamba JB atakuwa na generata.

Uvunjaji wa mila na desturi
Ingawa Nelly na Devi ni watu wakisasa bado wana familia zao zenye mil ana desturi tofauti. Katika harusi za Kitanzania, mila na tamaduni zina jukumu muhimu. Devi tayari amesha mkashirisha JB kwa kuamua kumoa Nelly bila baba yake JB kukubali. Je hilo litamletea laana?

Usikose kuangalia harusi ya Nelly na Devi ndani ya kipindi cha #MMBHuba kila siku ya wiki saa 3 usiku ndani ya DStv chaneli 160! Ni nani atavuruga harusi ya Nelly na Devi? Tuambie hapo chini 👇

Huba
Harusi ya Nelly na Devi - Huba

Ni nani atavuruga siku ya harusi?

Wana harusi (Nelly na Devi)13%
Wazazi (JB au Tesa)5%
Ma Ex (Kibibi au Tima)82%