Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Abby achangamsha #MMBHuba – Maisha Magic Bongo

Habari
14 Septemba 2023
Wakati Devi akiendelea kuwa mahututi Abby awasha moto mkali ndani ya Huba.
Article

Abou Zakitamim ajiunga na tamthilia ya #MMBHuba akiigiza kama Abby, Abby anakuja kwa kishindo kikuu , tukio lake la kwanza ikiwa ni  kumgonga  Devi na gari. Bi Sikitu allijikuta akituma majanga ya JB kwa Devi, kwa bahati mbaya kwa sababu ya hasira. Hili jambo lilimsababisha Devi kuingia kwenye ajali mbaya sana ambayo ilimuacha akiwa mahututi hospitalini. Wakati familia yake ikiwa inaomboleza na kusikitika, Abby alikuja hospitalini kujitambulisha kwa familia ya Devi na kuwaelezea yaliyo tokea.

Akiwa hospiali Abby anakutana  na Doris, nia  yake haswa ikiwa haijulikani ni nini Roy anahisi ana mipango potofu na Doris , na anautafuta ukaribu na ndugu na jamaa za Devi wa karibu kwa nguvu.

Mapokeo ya Abby katika kiindi cha #MMBHuba yalikua mazuri sana , soma machache waliyotiririka watazamaji hapo chini.

@teklachichi - "Huba imekua tamuu saivi hadi raha,,,na huyu handsome nani tenaaa,,kesho tukutane saa 3🔥"

@goychae- "Eeeeeh jmniiiiii this man namkubali since day one nimemuona tiktok 🥰🥰huyu c @abouzakitamim7 🥰😂😂usharud bongo au bado😁"

@lyidia_shoes @lyidia_shoes  - "Hii Huba kama nianze kufatilia tena😢😢😢Kuna mda nilisusa jamani wacha nirudii😂😂😂😂😂nipokeeni @lyidia_shoes @lyidia_shoes 👏"

@newbabyintheworld - "Hivi we director wa huba hawa wanaume wazuri huwa unawatoagi wapi??Yaani Huba ina wanaume wazuri balaaaa....Kuanzia Davy,Yakubu,Loi,JB,na huyu mwingine hapa ndo balaaaaa"

Huba
Abby - Huba

Je Abby ndiye atakaye fanikiwa kufanya Doris aachane na Roy?

Click here to make your selection
Ndiyo
Hapana

Endelea kufuatilia Tamthilia yetu pendwa ya  #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya DStv chaneli 160. Pia kumbuka kujiunga na #MyDStv App kuendelea kuburudika na tamthilia hiii #MMBHuba popote ulipo.