Wakati tunaazimisha siku hii ya miaka 60 ya uhuru, tunapenda kuwakumbusha vipindi bomba vya Kitanzania ndani ya Chaneli 160. Kianziazia asubuhi mpaka usiku unaweza kupumzika na kupata burudani za kipekee ndani ya Maisha Magic Bongo:
Danga saa 6 mchana (marudio)
Anza siku yako ukiburudika na kipindi cha Danga, marudio ya kipindi cha jana yatacheza saa 6 mchana. Hiki kipindi kinachohusu madada wawili, Angel na Pipi pamoja na rafiki yao wa kiume, Mo. Pamoja wanafanya kazi ya wakuwadhulumu matajiri chini Tanzania wakitumia urembo wao, akili na miunganisho yao. Kwa vipindi vipya usikose kuangalia kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 1:30 usiku.
Bass saa 11 jioni
Pata kipindi kipya cha Bass ambacho kitakuletea burudiani kwa njia ya muziki. Burudika na miziki ya kisasa ambayo inavuma sana kwenye chati. Pia unaweza kuangalia mahojiano na mastaa wa Bongo Flava wanaovuma nchini.
Harusi Yetu saa 1 usiku
Jiunge na mtangazaji wetu mpya, Precious Myner kwenye kipindi kipya cha #MMBHarusiYetu ambacho kitakuwa kinaonyesha harusi ya wiki hii. Burudika na harusi ya halisia ya kitazania kuanzia stori ya njisi walivyo kutana, angalia kitchen party, send off, harusi yenyewe mpaka ukumbini.
Huba saa 3 usiku
Huba ni kipindi kipenzi sana nchini Tanzania, kipindi hiki kina husu mapenzi na jinsi watu wanavyoweza kufanya ubaya na pia uzuri kutokana na huba. Jiunge nasi leo usiku kuangalia kama mahusiano kati ya Devi na Nelly yataendelea? Na je Tima atamuacha Jude?
Jua Kali saa 3:30 usiku
Kipindi cha Jua Kali kinahusu Professa Bill, ambaye pamoja na Thomas wanaendesha kampuni ambayo wanatumia kudhulumu watu. Wakati pia kukiwa na shida tofauti ndani ya familia za Bill na Thomas.
La Familia saa 4 usiku
Tamthilia hii inazungukia familia ya Bibi na Bwana Ibrahim, familia yao yenye watoto watano. Baada ya Bwana Ibrahim kumteua mtoto wake wa kwanza wakiume, Raphael, kuwa mkuu wa kampuni ya familia, binti yake wa kwanza Violeth akasirika na kuanza vita na familia.
Tunakutakia siku njema ya uhuru, na tunakushukuru kuendelea kuchagua Chaneli ya Maisha Magic Bongo!