Tesa yupo sehemu mbaya kwa sasa hivi baada ya kukopesha pesa toka kwa Kibibi na kushindwa kulipa. Kwa sasa, Tesa amepoteza kazi yake na kampuni yake na mahusiano kati yake na mwanae Devi yamekuwa mabaya baada ya Kibibi kutomruhusu Tesa kuja nyumbani kumwona Devi tangu ajali yake.
Tesa akiwa kwenye misukosuko ya kutafuta pesa, ajiingiza ndani ya mchezo ya wapiga ngumu ambapo anacheza kamari na watu wengine. Akiwepo hapo anakutana na kijana mmoja anaye mzidi umri, anayeitwa Diesel. Diesel ni rafiki yake wa zamani wa Nicole na Diesel adai kwamba anampenda Tesa na yupo tayari kuanza mahusiano naye.
Baada ya misukosuko Tesa aliyopitia alivyokuwa na Pedro, aanza kuwa na wasiwasi kwamba ataweza kweli kuwa na mwanaume kijana tena. Wakati pia, wasiwasi inakuja kwake ni kwanini Diesel anamtaka, je anafuata pesa tuu? Na hataki marudio ya matukio yalio mpata wakati alivyokuwa na Pedro. Je itakuwaje?
Fuatilia mahusiano ya Tesa na Diesel kwa Zaidi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa tatu kamili ndani ya Maisha Magic Bongo!