Logo
MMB HubaSM V1 TwitterCover Generic HR
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Mhalifu mkuu mwaka huu! - #MazuriYa21

Habari
17 Decemba 2021
Kuna watu ambao hatukuwapenda mwaka huu!
Untitled design (28)

Kuna waigizaji ambao walifanya kazi nzuri sana kwenye uigizaji wao mpaka tulianza kuwachukia! Hawa wailigizaji waliigiza kama wahalifu, watu amabayo tuliwachukia kwa jinsi walivyokuwa wakitesa wenzao. Hapo chini tumeanda orodha ya baadhi ya waigizaji ambao walikuwa wahalifu sana mwaka huu:

Frank (Jua Kali)

Kaka Frank alijifanya mabaya kwa Naira wakati akijifanya kuwa mtu mwema kwa wengine. Kisa cha kumtesa Naira ni kwasababu, alikuwa na mahusiano nae, akijua kwamba Naira anampenda na aliweza kupata mahusiano nae bila kuwa nae rasmi.

Kibibi (Huba)

Kibibi ni mkali sana, baada ya Ngote kufariki, aliamua kurudi Dar es Salaam na alianzisha mahusiano na Devi. Ingawa Devi alikuwa bado amemuoa Tima, Kibibi hakujali. Wakati Devi na Kibibi walivyokuwa pamoja, Devi alipata ajali mbaya ambayo ilimfanya awekilema. Kuanzia hapo Kibibi alianza kumtesa Devi kwasababu aligundua kwamba Devi alikuwa anaenda kumuona Tima kabla ya ajali yake.

Jemo (Pazia)

Jemo alionyesha kuwa alikuwa mtu mzuri baada ya kuonyesha upendo kwa Regina, lakini mambo yalifika pabaya baada ya watu kugundua kwamba hakuwa na pesa. Nalichofanya ni kuibia wadhamini wake wa chuo ili kuendelea kuishi maisha ya kifahari.

Jude (Huba)

Baada ya mke wake wa kwanza kufariki watu wengi walikuwa na wasiwasi kwamba Jude ndiye aliyekuwa muhusika wa kifo chake. Alivyona kwamba Tima aliachana na Devi, alichukua fursa hiyokumoa Tima. Baada ya ndoa, alianza kutesa na kumpiga Tima. Tabia ya Jude ilifikia pabay mpaka, akaua. 

Je kati ya hawa ni nani alikuwa mhalifu zaidi?

Mhalifu mkuu - #BestOf21

Nani alikuchukiza zaidi mwaka huu? Piga kura yako hapo chini

Frank (Jua Kali)15%
Kibibi (Huba)32%
Jemo (Pazia)7%
Jude (Huba)45%