Logo
MMB HubaSM V1 TwitterCover Generic HR
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Mchepuko apewe zawadi ya sikukuu ya wapendanao?

Habari
11 Februari 2022
Watazamaji wa Maisha Magic Bongo watoa maoni kama michepuko wapewe zawadi ya Valentine!
Screenshot 2022 02 09 at 17

Sikukuu ya wapendanao inakaribia, na siku hii inasherekea mapenzi ya aina tofauti. Ndani ya vipindi vya Maisha magic Bongo kuna mapenzi ya tofauti, tumeona jinsi mtu kama Kibibialivyofanikiwa kuwa mke wa Devi baada ya kuanza kama mchepuko wake. Baada ya kufunga ndoa, Devi alianza mahusiano na mchepuko mwingine, Nelly.

Na pia kuna mtu kama Maria wa Jua kali, Maria ana wanaume wengi kuanzia Lukas, Felix na pia baba yake Felix, Thomas. Tatizo kubwa la Maria kwa Thomas ni kwamba Thomas tayari ana mke, Stella.

Ukiangali Sinia pia kuna, Sharifa amabaye ni mchepuko wa wanaume tofauti. Kwa sasa hivi anaujauzito lakini hatujui mimba ni ya nani?

Sasa kwenye maswala kama haya, ni lazima kuwapa zawadi kwenye sikukuu hii ya wapendanao? Angalia watazamaji wetu wamesema nini hapo chini:

@simonupendoΒ - "Wapewe mimba tu inawatoshaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚"

@magawamakombaΒ - "Duhhhh KWA wtz bora zawadi akose mke sio mchepuko."

@anna_8453Β - Lazima tena sana Kama majukumu anayatekeleza vyema au anapendwa why asipewe Zawadi tena hawa wanajikusanyiaga Zawadi kuliko mmilikiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚"

@platinamujrΒ -"NdioπŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»"

@dad_dotaΒ - "Mbona michepuko watapewa na wenye Mali watabaki wapigwa na jua tu"

@bellazaujathΒ - "Ndio ni lazima kwani vp.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜’"

Je na wewe unakubaliana nao? Tuambie hapo chiniΒ πŸ‘‡

Untitled design (8)
Sikukuu ya wapendanao!

kama mtu ni mchepuko ni lazima apewe zawadi kwenye sikukuu ya wapendanao?

Ndiyo, apate!63%
Hapana, asipate!37%

Mengine zaidi:Β 

Β