Logo
MMB HubaSM V1 TwitterCover Generic HR
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Malengo ya wahusika wa Huba ndani ya mwaka 2022 – Huba

Habari
20 Januari 2022
Mwaka Mpya, mambo mapya!
Untitled design

Tangu mwaka mpya ulivyoanza kila mtu anamalengo yake na jinsi wangependa mwaka huu uwe tofauti na mwaka jana. Kuna watu ambao walikuwa na mwaka mzuri na wengine ambao mwaka wao ulikuwa sio mzuri sana. Kwa wale waliokuwa na mwaka mzuri mwaka jana wangependa kuboresha, na wale waliokuwa na mwaka mbaya mwaka jana wangependa kuwa na mwaka mzuri zaidi. Hapo chini kuna malengo tofauti ndani ya wahusi wa Huba:

  1. Doris

Lengo kubwa kwa Doris mwaka jana lilikuwa kuolewa na Roy. Ingawa Roy hakumuacha Nandy, aliwaoa wote wawili. Kwa sasa hivi, Doris ana mimba na lengo lake kubwa mwaka huu ni kumzalia Roy mtoto. Je atafanikiwa?

  1. Happy na Chidi

Mwaka jana, lengo kubwa kwa Chidi na Happy lilikuwa kufunga ndoa na hatimaye walifunga ndoa. Kukaribia mwisho wa mwaka, Chidi na Happy walikuwa na malengo ya kuhama kutoka nyumbani kwa Tima iliwaanze familia yao. Lakini baada ya Jude kuanza kumtesa Tima, waliamua kubaki, je watatoka kwa amani?

  1. Devi

Mwaka jana haukuishia vizuri kwa Devi, baada ya kumuacha Tima alipata ajali mbaya sana ambayo ilimfanya mguu yake ipooze na hakuweza kutembea. Baada ya kutoka hospitali, ndoa yake na Kibibi ilizidi kudidimia na Kibibi alizidi kumtesa. Hatimaye alipata daktarin, Nelly, wakumsahidia. Je Devi ataweza kutembea mwaka huu?

  1. Tima

Mwaka jana haukua mzuri kwa Tima, Devi alimauacha ili aende kwa Kibibi. Baada ya kuacha, Tima alianza mahusiano na Jude, na Jude alianza kumtesa. Tima alijuka kwamba amekwama ndani ya mahusiano yake na Jude. Malengo yake mwaka huu ni kuachana na Jude, je ataweza?

Kumbuka kuangalia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya DStv chaneli 160!