Baada ya miaka mingi, hatimaye Jude alifanikiwa kumpata mwanamke wa ndoto zake, Tima. Hii sio ndoa ya kwanza ya Jude, na pia Tima sio ndoa yake ya kwanza. Kabla ya hawa wawili kuoana Jude alikuwa alishawahi kumuoa Rani, na ingawa hakuna ushahidi, watazamaji wa #MMBHuba wanajua kwamba Jude ndiye aliyemuua Rani. Kwa Tima pia,bahati mbaya ilikuja baada ya mume wake Devi kutekwa kimapenzi na Kibibi na hili jambo lilimfanya amuache Tima. Kipindi Tima alivyokutana na Jude, alikuwa amevungika moyo na Jude alijionyesha kwake kama mtu ambaye ataweza kuuponesha moyo wake. Lakini, baada ya ndoa tuu, mambo kati ya Jude na Tima alianza kudidia na Jude alianzakumtesa Tima.Hapo chini ni baadhi ya mambo Jude alimfanyia Tima.
Kumuoa kwa haraka
Alivyojifunza kwamba Devi alikuwa na mpango wa kumuacha Tima, moja kwa moja Jude alijiingiza ndani ya Maisha ya Tima.
Kumuondolea Tima ndugu zake na watoto wake
Baada ya Jude kuona kwamba Tima alianza kumkumbuka Devi na kuhisi kwamba Tima bado alikuwa na hisia kwa Devi, Judealikasarika sana. Aliamua kumlazimisha Tima kuwaweka watoto shule ya boarding na kumpiga marufuku kuona baba yake na Sidi.
Kuanza kumpiga
Tim ani mwanamke mwenye nguvu san ana Jude, aliona kwamba haikutosha kuondelea kila kit una alianza kumpiga. Kila akikasirika aishia kumpiga na baada ya siku arudi kuomba msamaha akiwa na zawadi. Hili jambo limemfanya Tima kujihisi kuwa mpweke na kuishia kunywa pombe kila siku.
Mambo yamefika pabaya, na Tima ndiye anaweza kujiokoa mwenyewe. Je unafikiri ataweza kumuacha Jude kabla Jude ajamfanyia Tima vile alivyo mfanyia Rani? Usikose kuangalia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya DSTV chaneli 160, Maisha magic Bongo.