Baada ya ajali aliyoipata wakati alivyokuwa akienda kumuona Tima. Devi aligundua kwamba Tima alikuwa anaolewa na Jude. Baada ya kuwa na mahusiano na Kibibi kwa muda, alitambua kwamba hisia zake kwa Kibibi hazikutoka ma bado anamtaka. Wakati alivyokuwa anaelekea kuvuruga harusi ya Tima na Jude alipata ajali mbaya mbayo aliumia miguu na hakuweza kutembea tena.
Baada ya kutoka hospitalini, Devi alirudi nyumbani kwa Kibibi. Lakini Kibibi alikuwa ana hasira sana baada ya kukugundua kwamba Devi alipata ajali akiwa anaenda kumuona Tima. Hili jambo lilimfanya Kibibi kuanza kumtesa Devi kila siku nyumbani.
Kwa bahati nzuri, hospitali ilimpa Devi therapist, Dr Nelly, ambaye alikuwa anakuja nyumbani na kufanya mazoezi na Devi. Baada ya muda, Dr Nelly aona kwamba Devi ananza kuonyesha mabadirisho. Je Devi atapona?
Kumbuka kufuatilia kipindi cha #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya DStv chaneli 160 kugundua zaidi.