Logo
Doli Showpage
channel logo dark

Doli Armaanon Ki

160DramaPG13

Vurugu za akina Mama katika Doli Armano Ki!

Habari
28 Agosti 2018
Vurugu na vita vya akina mama ni sawa kila mahali duniani! Ukitazama akina mama wa wasanii wetu, Mama Dangote na Mama Mobetto, ni akina mama wagani katika kipindi cha #DOLITZ wanaweza kusawazishwa na hawa? SOMA ZAIDI!
<p>Doli Mums</p>

Katika maisha ya kawaida hapa Bongo,  tumeona na kushuhudia mengi yakiendelea huku na kule, kila mmoja akiwa na lake!  Mitandaoni, mama zetu pia wame trend kwa hili na lile. Waliotisha zaidi ni mama zetu Mama Dangote na Mama Mobetto!

Ukiangalia wamama hawa  wangetakiwa kuwa kitu kimoja kwa sababu watoto wao wamezaa pamoja, lakini, wameamua kukaa mbali na mizozano ya watoto wao na klila mtu kupambana na yake!

Wamama kama hawa pia tunawaona katika tamhilia ya DOLI ARMANON KI, mama yake URMI na Mama ISHAAN, wamama hawa ni kweli wanatofautiana sana. 

Wote wakitaka mema kwa ajili ya watoto wao , kwa namna zao tofauti, mama yake Ishaan hamtaki Urmi awe na mwanaye kabisa, sababu zake bado hazina mbele wala nyuma!  Anaungana na Samrat aliyekuwa mume wa Urmi zamani, wanakua kitu kioja ili kuwavuruga Ishaan na Urmi.

Wakati mama yake Ishaan anapanga yote haya, Samrat anakutana na binti yake na wao pia wanafunga ndoa. Kasheshe lingine hilo jameni! 

Kwa upande mwingine mama yake Urmi hana lingine zaidi, ila kuwatakia mema wote pande zote mbili.

Je nani anafaa kuwa Mama Dangote na nani anafaa kua Mama Mobetto kati ya mama Ishaan na mama Urmi?

Pata video ya yaliomo wiki hii katika Doli Armano Ki!