Manga Diwani
Manga ana umri wa kuelekea miaka ya kati ya 50, ni mume wa Dida, baba yake Yaz na pia mkwe wa Hamza na Azra. Yeye ni bosi wake na Hamza na pia marafiki yake toka utoto. Mzee Manga ni msanifu wa majengo na nikibosile mkubwa ndani ya biashara yake.
Dida Diwani
Dida ana umri wa kuelekea miaka ya kati ya 40, na ni mke wa Manga, mama yake Yaz na mkwe wa Hamza na Azra. Dida ni mama wa nyumbani na anapenda sana kujishughulisha na shugli mbalimbali, ni mama mwenye cheo na kwake hilo swala ni muhimu sana.
Yaz Diwani
Yazi ni kijana wa umri wa miaka 25, yeye ni mtoto pekee wa Mangana Dida, mkwe wa Hamza na mume wa Azra ingawa waliachana. Ni kijana msomi na mwenye msimamo.
Hamza Shakombo
Hamza umri wa kuelekea miaka ya kati ya 50, ni baba yake Azra na mkwe kwa Manga, Dida na Yaz na baada ya Azra kuolewa tena alikuja kuwa baba mkwe kwa Shem pia. Ni mfanya kazi kwenye kampuni ya Manga n ani mshauri wake mkuu.
Azra Shakombo
Azra ana umi wa miaka 25, ni binti yake na Hamza na mkwe wa Manga na Dida. Ingawa yeye na Yaz wamepeana talaka, bado wanaukaribu. Azra ni mwanamke mzuri na analinda familia yake na pia ni mtu muaminifu.
Shem Baharia
Shem ana umri wa kuelekea miaka ya kati ya 30, ni mume wa kwanza wa Mishi na baada ya kuachana na Mishi alimuoa Azra na kuwa mkwe kwa Hamza. Yeye ni mfanyakazi wa baharini na anapenda kusafiri sana.
Mishi
Mishi ana umri wa miaka 30 na ni mke wa kwanza wa Mishi. Yeye ni mtu anayependa kutoka sana na Shem alimua kulinda radhi yake ndani ya jamii lakini wakati alivyokuwa kwenye ndoa nae alitembea na wanaume wengine na ndio maana Shem aliamua kumuacha. Mishi achukia kwamba Shem aliamua kumuoa Azra.
Rukia
Rukia ana umri wa miaka 25 na ni mtoto yatima. Yeye ndio rafiki wake wa karibu sana na Azra na ni mke wa Babaz. Anafanya kazi ya ufundi na pia anapenda sana kupiga stori.
Babaz
Babaz ana umri wa kuelekea miaka ya kati ya 30, na ni mfanyakazi wa baharini. Yeye ni mume wa Ruki ana pia ana biashara na Shem.
Jiunge nasi kuanzia Jumatatu tarehe 2 Oktoba saa 1:30 usiku kukutana na hawa watu wote ndani ya #MMBChanda.
Kumbuka kwamba unaweza kujiunganisha na #MyDStv App popote ulipo kuburudika na vipindi vyote vya #MaishaMagicBongo. Mengine: