Logo
Chanda
channel logo dark

Chanda

160DramaPG13

Familia tatu ndani ya #MMBChanda – Maisha Magic Bongo

Habari
29 Oktoba 2023
Pata kujua historia ya familia zinazoongonza ndani ya kipindi cha Chanda.
Chanda

Familia ya Diwani

Manga Diwani ni mfanya biashara na tajiri sana. Manga alikulia kwenye hali ngumu tangu utotoni lakini alipata bahati baada yakukutana na Dida kwenye sherehe iliyoandaliwa na familia ya Dida. Baada ya miezi sita ya kujuana na Dida, alifunga ndoa, familia ya Dida ndio iliyo msaidia kujenga kampuni yake ya usanifu wa majengo. Baada yam waka mmoja ndani ya ndoa yake na Dida, Yaz alizaliwa, na Manga alihakikisha kwamba mtoto wake hata kuwa lolote lisilo mtosha maishani mwake mwote. Baada ya Yaz kutimiza miaka 25, aliamua kumuoa Azra mtoto wa Rafiki yake Manga, Hamza. Ingawa Manga hakupenda hiyo ndoa, aliamua kumkubalia mwanae kumuoa Azra.

Familia ya Shakombo

Hamza ni Rafiki yake wa karibu wa Manga na walijuana tangu utotoni na walipitia mengi pamoja. Hamza alipewa kazi ya upishi nyumbani kwa Manga baada ya Manga kumuona akiwa anahangaika na Maisha, lakini Dida hakufurahia kumpa Hamza kazi kabisa. Kipindi Hamza alivyoanza kazi hiyo, alikuwa maeshaoa na pia na mtoto mmoja anayeitwa Azra. Kipindi Azra alivyotimiza miaka mitano, Hamza aliamka kugundua mke wake amemtoroka na kuanzia hapo aliamua kumwambia Azra kwamba mama yake alifariki. Baada ya Azra kutimiza miaka 23, Hamza alirudi nyumbani kumwambia kwamba Manga Diwani alitaka aolewe na kijana wake, Yaz, na kwa kumshangaza Hamza, Azra alikubali.

 

Familia ya Baharia

Shem Baharia ni mfanyakazi wa baharini na kwasababu ya kazi yake ana safari sana. Miaka iliyopita aliwahi kumuoa Mishi, Mishi ni mwanamke mwenye fujo sana na kwa kweli alimpenda. Kipindi Shem alivyomuoa Mishi, alikuwa akifiria kwamba baada ya ndoa yao angetulia kidogo lakini Mishi aliishia kutembea na wanaume wengine wakati alivyokuwa na Shem na ikaishia na Shem kumpa talaka. Baada ya kuachana na Mishi, Shem aliamua kama akioa tena, ataoa mwanamke bikira.

Endelea kufuatilia hizi familia tatu kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku kupitia DStv chaneli 160!