Kuna haja ya mapumziko baada ya siku nzima ya mishemishe, na sisi kama Maisha Magic Bongo tunatambua hilo na ndio maana tunakuletea burudani inayonoga kupitia Asumanii Vibes : kipindi cha Muziki kinachoeendeshwa na Mkali wa MaDjs ; DJ Ally B almarufu Asumaniiiiiiiiiii.
Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatatu hadi Alhamisi saa 11 jioni ndani ya Maisha Magic Bongo na kina malengo ya kukutuliza, kukuburudisha na kukujuza yaliyomo kwenye Dunia ya Mziki, lengo kubwa likiwa kwenye mziki wetu wa hapa Nyumbani Tanzania.
Kuhusiana na Ally B
DJ Ally Bi ni mmoja wa DJs maarufu Afrika Mashariki na anajulikana kwa ustadi wake wa kipekee wa kuchanganya muziki, kupiga miluzi na sarakasi za kuchekesha. Ana mazoea ya kutumia matamshi ya, ‘Maneno Machache, Pesa Nyingi!' na 'Brothers and Sisters! Ladies and Gentlemen! Nasemaje! Nasemaje!'. Ninauhakika umekutana na maneno hayo kwenye mtandao, sio?
Hivo basi, tunakukaribisha kutazama 'Asumani Vibes' kila Jumatatu hadi Alhamisi saa 11 Jioni ndani ya Maisha Magic Bongo (DStv 160)
“Nasemajee! Nasemajeee! Maneno Kidogo, Pesa Nyingi.”