channel logo dark
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Ngote and Kibibi:  Wanandoa Wa Kali Sana Ndani ya Huba

Habari
17 Septemba 2020
Ngote and Kibibi wameweza kufanikiwa ki binafsi, lakini pamoja wamekua moto ambao haushikiki.
Ngote na Kibibi Article

Watu wengi hawakuweza kuelewa uhusiano kati Ngote na Kibibi mwanzoni. Tatizo la kwanza ulikuwa umri, umri wa Ngote ni mara mbili na umri wa Kibibi. Hilo swala lilifanya watu wengi wasikubali ndoa yao, lakini hawakusikiza na wamefanikiwa kujenga ndoa imara na kuwa na maisha mazuri pamoja. Pia bila kutosahau washabiki wa #HubaTZ wengi wanaendelea kupenda sana ndoa yao.
 


Sio siri kwamba Kibibi alikuwa ameolewa na Chidi, kipindi alivyokutana na Ngote. Chidi alimpenda sana Kibibi, lakini Kibibi alimwona Chidi kama njia ya kupitia ili apate mwanaume tajiri. Tangu zamani Kibibi ni mtu aliye kuwa akipenda vitu vya kifahari, na tangu Chidi alikuwa anawafanyia kazi watu matajiri, Kibibi aliona kama ndio upenyo wake kuingia kwenye hayo maisha. Na alikuwa na haki sababu alivyoolewa na Chidi tuu, akakutana na Ngote.

Alivyokuwa na Ngote, Kibibi alijikuta akiishi maisha ya kifahari na akajua kwa uhakika kama Ngote ni mwanaume aliyekuwa anamtafuta maisha yake yote. Baada ya muda, Ngote na Kibibi walifunga ndoa na pia Kibibi akazaa mtoo wa kike, Angel. Hatimaye, Kibibi akagundua ni jinsi gani Ngote anatengeneza pesa na jinsi gani aliweza kuwa tajiri. Aligundua kwamba Ngote anafanya biashara za uhalifu na madawa ya kulevya. Hiki kitu hakimuogopesha Kibibi. Akaamua kwamba na yeye pia anataka kujishugulisha na biashara hizo ili Ngote akifariki awe mkuu juu ya hizo biashara. Swala hili haliku mfurahisha, Miraj, mtoto wa kiume wa Ngote toka kwenye ndoa yake ya kwanza. Miraj alikasirika na akaanza kumchukia Kibibi na kumuweka yeye na mdogo wake, Angel kwenye hatari.

Kwa hayo yote yaliotokea, Ngote na Kibibi hawajawahi kuachana. Wamezidi kuwa na uhusiano wa “kufa na kufaana” na jukumu lao kubwani kujenga himaya kubwa pamoja.
Usikose kuangalia vipindi vyipya vya #HubaTZ kila Jumatatu mpaka Ijumaa saa 1 usiku na marudio kila Jumamosi saa 10:30 ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.