Kwa jinsi Nandy na Roy walivyopendana hakuna mtu aliyeweza kutegemea kwamba hatimaye wangeachana. Lakini, yalitokea na baada ya Nandy kufikiria kwamba Roy alikuwa na Doris kwenye usiku wa kuamkia harusi yao aliamua kutimua na kuondoka kukwepa aibu yeyote.
Kama watazamaji, sisi tunajua kwamba huo haukua ukweli lakini baada ya Nandy kuondoka, roho ilimuuma sana Roy. Na yeye kuwa binadamu na pia kuchanganya na historia yake na Doris, aliamua kurudiana na Doris.
Wakati akiwa kijijini, Nandy akutana na Yakubu na waanza mahusiano. Penzi lao lilipitia changamoto kubwa baada ya mume wake wa kwanza wa Nandy, Konde, kurudi kijijini. Nandy aliachana na Konde baada ya Konde kumnyanyasa wakati walivyokuwa ndani ya ndoa yao. Konde alimteka Nandy Pamoja na dada yake Yakubu, Sada, lakini hatimaye Yakubu aliwaokoa na kukuhakisha Konde hawezi kumuumiza Nandy tena.
Baada Nandy kuwa huru, yeye na Yakubu walianza mpango wa kuanza safari ya kurudi mjini. Taarifa zikamfikia Roy, ambaye bado amemuweka Nandy moyoni mwake. Kurudi kwa Nandy kumeleta matitizo makubwa ndani ya uhusiano wa Roy na Doris kwasababu Doris anaanza kuona wivu akidhani kwamba Nandy na Roy watarudiana.
Fuatilia tamthilia yetu ya #HubaTZ kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160!
