Mwanida anajikuta kwenye hali ngumu baada ya Frank kuanza kuhisi mtoto si wake . Wasiwasi huu unaweza kutikisa ndoa na familia yao nzima.
Wakati huo huo, Lindiwe anaingia kwenye malumbano makali na binti yake Bupe kuhusu pombe . Lakini majibu ya Bupe yanatikisa zaidi — anasema chanzo cha ulevi ni mama yake mwenyewe! Familia ya Nguzu inazidi kuyumba huku kila siri ikileta maumivu mapya.