Roma anaona uso wa Balraj na kushtuka. Kumbumbu zote za zamani zinakuja na wakati anataka kujificha Balraj anamshika mkono wake na kumkabidhi kwa wanaume wenzake na kumteka nyara. Wanaendelea kunyua huku wakifurahi kwamba wanaenda kuvuruga harusi ya Padmini.
Madhu na Trish wanasaidia Padmini kuchagua mavazi ya harusi na kumfanya awe tayari na kila mapambo. Baada ya matayarisho,familia nzima inaondoka na kuelekea kwenye ukumbi wa harusi.
Wakati wanafika huko, Madhu anajaribu kupiga Roma lakini simu yake iko mteja. Anaamua kumpigia RK na kumsimulia ndoto ya Padmini kuhusu Balraj.
Madhu anakata simu wakati BSC anaingia na wanaume wenzake. Amevalia nguo za bwana harusi huku akiekelea kwa Padmini. Balraj anaendelea kumkaribia Padmini na hapo aka fichua uso wake.
Kila mtu anashtuka. Balraj anachukua bunduki na kuielekeza kwa Padmini. Anaamrisha wanaume wenzake kufunga wageni wote walioko kwa harusi. Madhu anaigilia kati na bishana na Balraj. Baljaj anamfunga kamba Madhu shingoni, tayari kumuangamiza.
Wakati anataka kumuua Madhu, RK anawasili na kumuokoa. Katika kasheshe hio, Padmini anachukua bunduki na kumpiga risasi Balraj. Je, huu ndio mwisho wake?
Picha zaidi hapa:
Fuatilia Madhubala kila Jumatano na Alhamisi ndani ya MMBongo pekee!
