channel logo dark
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki13

Malkia wa Mitindo ya Nywele Waanguka

Habari
20 Agosti 2020
Kifo cha Rani na Ruki kimeleta giza sana kwenye msimu huu wa Huba, ila waigizaji Regina Mroni (Rani) na Christina Mroni (Ruki) alileta mwanga kwenye mitindo yake ya nywele zake halisi.
Huba Hair Article

                                                                                                                                                                                                    Nywele kwa mwanamke wa kiAfrika ni kama taji, wanawake wa Huba wanatuonyesha mitindo mingi ya nywele kila wiki. Wiki hii tulipendelea kuwapa kipao mbele Regina Mroni na Christina Mroni.
Huba inaendelea kuwa kwenye majonzi ya Rani na Ruki, kifo cha Rani kimekuja kwa ghafla bila kutarajiwa ikiwa mauti yalimkuta kutokana na mipango yake na dada yake kugonga mwamba na Rani kuishia kunywa kinywaji chenye sumu, na kifo cha Ruki kimesababishwa na mume wake Jude. Ukiacha vipaji vyao, warembo hawa walituvutia sanana mitindo mingi mizuri  ya nywele.

1. Kuosha na kuchana
Huu mtindo ni rahisi sana, tunaupenda kwa sababu  baada ya kuosha nywele unaweza kuzichana tuu na kuendelea na siku yako.
 

2. Kuchana upande mmoja
Tunaupenda sana mtindo huu kwa sababu unaweza kuuva na kuoneka umetoka lakini bado unavutia sura yako kwasababu sura inaonekana vizuri.
 

3. Kidoti cha juu
Kubana kidoti juu ni safi sana tunapenda mtindo huu, kwa sababu unaweza kuuva mchana toka ofisini na usiku ukitoka pia bila kubadirisha.

4. Kilimanjaro
Tunapenda mtindo huu kwa sababu unalinda nywele na kusahidia nywele kukua
 



5. Mabutu laini
Kama mfumo wa vitungu, mitindo huu nikufunga mabutu laini kama vitunguu na kuachia, tunapenda jinsi mtindo huu hausumbui nywele sana.


7. Kuchana na kuachia
Tunapenda mtindo huu sababu unaruhusu mtu kuonyesha jinsi nywele zake zikwa na afya nzuri akiachia tu.
 

Usikose kuangalia kipindi cha Huba kila Jumatatu mpaka Ijumaa saa 3 kamili usiku, ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160 pekee.