channel logo dark
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Wanaume wanaompenda Maria – Jua Kali

Habari
30 Septemba 2021
Mwanakondoo Maria ameumiza mioyo mingi nah ii ndio orodha ya wanaume wanaompenda.
Screenshot 2021 09 30 at 16

Felix

Felix ndiye mwanaume wa kwanza kuonyesha mapenzi kwa Maria na alikuwa na hamu ya kumuoa lakini baada ya kumleta Maria nyumbani, aligundua kwamba Maria alikuwa aktembea na baba yake Thomas.

Thomas

Mr Thomas AKA “madevu” alimpenda Maria wakati alivyokuwa akifanya kazi ofisini kwake. Ingawa Mr Thomas alikuwa ameshaoa halikumfanya amuache Maria. Baada ya mke wake, Stella, kugundua mahusiano yao alijaribu kumuacha Maria lakini anadai kwamba bado anampenda.

Luka

Luka alikuwa anasali na Maria, baada ya muda alianza kumpenda na wakaanza mahusiano mpaka aka mvisha pete ndani ya kanisa na Maria akakataa. Luka anadai kwamba yeye bado anampenda Maria, aliamua kumleta mama yake kumsahidia kuongea na Maria na Maria alikataa.

Frank

Baada ya kuchoka kumchezea Naira, Frank aliamua kuzidisha mahusiano yake na Maria. Walikutana ofisini na Mary anajitahidi kuficha mapenzi yake na Thomas wakati akiwa na Frank.

 

Fuatilia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku kujua Maria ataishia na nani.