channel logo dark
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Stella afumwa chumbani kwa Felix – Jua Kali

Habari
28 Oktoba 2021
Baada ya kujikuta chumbani kwa Felix, Stella hajui atatoka kivipi bila Thomas kumuona.
Screenshot 2021 10 28 at 12

Ndoa ya Thomas na Stella iko mashakani baada ya Stella kugundua kwamba Thomas alikuwa na mahusiano ya siri na mchumba wa mtoto wake Felix, Maria. Alivyogundua hivyo, Stella alijaribu kuokoa ndoa yake, kwa kumwambia Maria achane na mume wake baada ya kumpiga na kumuweka hospitalini.

Baada yah apo Thomas aliomba msamaha kwa mke wake, Stella. Thomas alisema kwamba alikuwa na nia ya kuimarisha ndoa yao. Kumbe huko kwake anaficha siri zake. Siri yakwanza ni kwamba bado ana mpenda Maria, nay a pili ni kwamba alizaa mtotona Suzanne.

Stella alianza kuwa karibu na Felix kwasababu ya ndoa yake kudidimia. Stella alijikuta akiwa chumbani kwa Felix wakati Thomas yupo nyumbani. Je Mr Thomas atawafuma?

 

Fuatilia stori hii kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku!