channel logo dark
Season 14
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Tunasherekea wakina mama ndani ya #MMBHuba

Habari
06 Mei 2021
Kwenye siku ya wakina mama tunasherekea wakina mama ndani ya Huba na jinsi wanavyo linda watoto wao.
Untitled design (14)

Hakuna pendo linalo zidi la mama, ingawa hawa wanawake ndani ya #MMBHuba wanakuwaga na tabia mbaya au wanapenda kufanya mabaya lakini bado kitu kimoja ambacho ni muhimu kwao. Hiki kitu ni jinsi wanavyolea watoto wao.

Tesa

Ingawa Tesa amefanya maovu mengi, ukiangalia ni kwanini anafanya haya yote ni kwasababu ya mwanae, Devi. Tatizo kubwa ni kwamba Devi alimuoa Tima bila ruhusa ya mama yake, hili jambo lilimfanya Tesa amchukie Tima kwa miaka yote na mpaka sasa bado anataka Devi na Tima wasiwe Pamoja.

 

Mama Annette

Mama Annette amefanya chochote ili Annette afurahi. Tangu Annette alivyoanza mahusiano na Pedro, mama yake alipenda sana. Lakini alipogundua kwamba Tesa bado anamtaka Pedro, aliamua kumteka Tesa hospitalini ili Annette na Pedro waendelee na mahusiano yao.

 

Kibibi

Kibibi ni mama yake na Angel, kipindi Kibibi alivyobebeba mimba ya Angel alikuwa ameolewa na Chidi. Tazizo kubwa lilikuwa kwamba, Chidi alikuwa hana pesa na alikuwa anataka kumlea mtoto wake ndani ya mazingira mema. Kibibi aliamua kumuacha Chidi na kumuoa Ngote ili mwanae apate maisha mazuri.

 

Tima

Tima na Devi walijaliwa watoto wawili baada yam toto wao wa pili kuzaliwa walianza kupata matatizo ndani ya ndoa yao. Haya matatizo yalimfanya Devi amuache Tima na watoto wao ili aende kuishi na Kibibi na Tima alibaki kuwa mama na baba wa watoto wote peke yake.

Fuatilia thamthilia ya #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.