Mapenzi kati ya Roy na Doris yametokea mbali, walisha wahi kuwa mme na mke na wakaachana. Kuachana kwao hakukua kwa kupenda kwa Doris ila palikua kwasababu Roy hakutaka tena.
Baada ya kuachana na Doris, Roy alikutana na Nandy na alimpenda sana. Kipindi alipokuwa na Nandy alimsahau kabisa Doris lakini, sio maana kwamba Doris nay eye alimsahau Roy. Alijaribu kwa mbinu yote kurudiana na Roy lakini Nandy alikuwa ameshamteka Roy. Kwa ujanja wake, Doris alikuja na mbinu mpya kabla ya harusi ya Roy na Nandy. Alifanya vituko vyake vyote ili Nandy aamini kwamba Roy alirudi kwa Doris. Kwasababu Nandy alikuwa tayari hamuamini Roy, mchezo wa Doris ulikuwa rahisi sana. Siku ya harusi Doris alimdanganya Nandy na bila kufikiria mara mbili Nandy akaamua kutoendelea na harusi na akatoroka kijiji kwa shangazi yake kumwacha Roy mpweke.
Kwa kweli Doris Alisha, na Roy kuwa kwenye hali mbaya na maumivu ya moyo akamamua kurudiana na Doris. Lakini sasa hivi akili inaanza kumrudia Roy, anaanza kumkumbuka Nandy na Doris and hisi kama hampendi tena. Je Doris anaweza kuvumia hii hali au nay eye atafika sehemu atashindwa na mapenzi?Usikose kuangalia #HubaTZ kila jumatatu mpaka Ijumaa ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160
