Logo
Chanda
channel logo dark

Chanda

160DramaPG13

Tamthilia mpya ya Chanda kuanza kurindima Ndani ya Maisha Magic Bongo

Habari
05 Oktoba 2023
Imejaa visa mikasa na matukio ya kusisimua; waigizaji wawataka watazamaji kukaa mkao wa kula.
Chanda

Safari hii itavuka soksi na kiatu kubaki mguuni kwa washabiki wa tamthilia pale tamthilia mpya ya Chanda itakapoanza kutikisa Ndani ya Chaneli ya Maisha Magic Bongo kuanzia Jumatatu Oktoba 2, 2023 saa 1:30 jioni.

 

Itakuwa ni patashika nguo kuchanika ndani ya tamthilia hiyo mpya iliyosheheni waigizaji maarufu na wenye mvuto kama vile Mwijaku, Feza Kessy, Hidaya Njaidi, na wengineo wengi pale watakapoonyesha umwamba wao wa kuigiza husa ukizingatia haditi inayobebwa na tamthilia hiyo iliyojaa vituko, visa, Mikasa, vitimbi na mikiki mikiki kutoka kwa waigizaji hao maarufu.

 

Kwa mara ya kwanza itaoneshwa kuanzia Jumatatu, tarehe 2 Oktoba saa 7:30 PM DStv katika Channeli namba 160, mfululizo huu wa tamthilia unatazamia kuwavutia watazamaji na mfululizo wake wa matukio ya kusisimua, wahusika wa ngulina wenye mvuto, na hadithi inayoakisi hisia za watazamaji wake. Huku vipindi vikionyeshwa Jumatatu hadi Jumatano, Chanda itakuwa dozi ya mapema ya usiku kwa wapenda tamthilia.

Msimu wa kwanza wa Chanda unaelezea maisha magumu ya Yaz Diwani, (Christopher Moris) na Azra Shakombo (Fezza Kessy). Akiwa amezaliwa katika familia tajiri na iliyoyukuka, Yaz, mrithi pekee wa himaya ya Diwani, anajikuta katika kimbunga cha penzi zito na Azra, binti wa mpishi na rafiki mwaminifu wa baba yake, Hamza Shakombo (Jafary Makatu). Muungano wao, ulioadhimishwa na harusi kuu ya Kiswahili ya yacht, inaonekana kama ndoto. Hata hivyo, chini ya kapeti, siri inatutumka

Presha inavyozidi kuongezeka, hasa kutoka kwa Dida Diwani (Hidaya Njaidi), mama yake Yaz, ambaye anatamani mjukuu, wanandoa hao wanakabili majaribu ambayo yanapima uhusiano wao. Huku Yaz akitunza siri nzito na uaminifu usioyumba wa Azra wa kumlinda, uhondo huu unaibuka kwa njia zisizotarajiwa na za kusisimua.

Barbara Kambogi, Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, anasema, "Tunafuraha kubwa kuwasilisha Chanda kwa watazamaji wetu. Hii sio tu tamthilia ya kawaida, ni mfano wa vipaji vya maridhawa tulivyonavyo. Waigizaji wetu ni bora zaidi. tunaamini Chanda itaweka alama katika tasnia hii kwa kuwa burudani bora kuwahi kutokea.

Picha: Barbara Kambogi (Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo)

Endelea. kufuatilia kipindi cha #MMBChanda kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya DStv chaneli 160!