Ndani ya vipindi vya Maisha Magic Bongo tuliona jinsi wanandoa na wapenzi wengi walivyokuwa sio waaminifu ndani ya ndoa zao. Tumekuandalia orodha ya watu waliokuwa kwenye mahusiano ambapo hawakuwa waaminifu. Soma hapo chini na tusaidie kuchagua:
Mishi (Chanda)
Ingawa Mishi ameolewa na Shem, sio mke mwema. Shem ni mbaharia anayefanya kazi kwenye meli na Rafiki yake Babaz. Wakati mume wake akiw kazini, Mishi anayefahamika kama “Malkia wa Huba” amekuwa akienda mjini na wanaume tofauti.
Harry (Wimbi)
Tangu mwanzo Harry amekuwa aeleweki na mekuwa akichezea wanawake watatu.
Maria (Jua Kali)
Kutoka kwa Lukas mpaka kwa Frank, Maria amekuwa na mahusiano na Thomas muda wote. Sasa hivi amepata ujauzito, je itakuaje?
Pili (Kitimtim)
Baada ya kumuacha Zunde, Pili aridu kwa Zunde na Zunde akaondoka na alivyorudi alimkuta Pili akiwa na Sabafu. Lakini kwa sasa Pili anaujauzito na ana mume mpya tena.
Henry (Jua Kali)
Baada ya Eliza na Miriam kumgombania, waligundua kwamba Henry ana mahusiano na mtoto wa Eliza, Gloria ambaye mwishoni alimuacha ili awe na Lolita.
Nicole (Huba)
Baada ya muarabu kumuacha, Nicole aliendelea mapenzi yake na Jude na akapata ujauzito kabla ya kumtoroka.
Endelea kufuatilia #MaishaMagicBongo tukiendelea kuhesabu matukio mazuri makubwa mwaka huu ndani ya #BestOf2023
