maisha magic bongo logo

Filamu zinazo sherekea baba wazazi ndani ya mwezi huu

Habari09 Juni 2023
Tunasherekea baba wazazi kila Alhamisi saa 8 mchana.
Article

Mwezi wa Juni tunasherekea baba zetu ndani ya Maisha Magic Movies. Soma orodha ya filamu zinazo angazia nguvu, umuhimu na nafasi ya baba mwezi  huu:

Visasi - 8 June

Baada ya mbakaji na muuaji wa mke wake kutoka gerezani, mume wake ajaribu kulipiza kisasi ili kupata heshima iliyopotea kwa mke wake.

Alifu kwa Ujiti – 15 June

Filamu hii inahusu mwanaume mlevi aliyekasirika analaumiwa kwa utekaji wa wasichana mabikira waliotoweka baada ya kurejea nyumbani kutoka jeshini.

When the Gods Argue - 22 June

Murambi analenga kuwa kiongozi wa jumuiya ya imani za kidini za watu wake ambazo zinamuongezea matatizo, na kuzidishwa na mabishano yasiyoisha ya miungu isiyofanya kazi anayoiomba.

Lucky Got Lucky - 29 June

Robert alifanya kazi kwa bidii ilikujenga maisha yake, na anakutana na rafiki wa zamani ambaye aliachana na mpenzi wake, na inaishia na mfululizo wa matukio ambayo yatafungua kila kitu.

 

Burudika na  filamu hizi na zingine chungu nzima  kila Alhamisi saa 8 mchana ndani ya DSv chaneli 141.