Mwigizaji Mkude Simba

Kwenye exclusive na DStv, mchekeshaji Mkude Simba aongelea kuhusu rafiki yake aliyeaga Sharo Milionea

Ni miaka mitatu imepita toka mwigizaji na mchekeshaji Sharo Milionea afariki kwa ajali ya gari akielekea Tanga nyumbani kwao mwezi wa November.

Inaonekana kadri muda unavyozidi kuyoyoma ndio rafiki yake mkubwa ambaye ni Kitale anapata nafuu ya kuyasema mengi ya moyoni ambayo hakuweza kuyasema kipindi kilichopita kutokana na machungu.
 
Kwenye exclusive na DStv.com Kitale maarufu kama Mkude Simba amesema anakumbuka ilibaki nusu aamini kwamba rafiki yake mkubwa Sharo Milionea amekua akitumia nguvu za kishirikina ili ang'ae zaidi kwenye sanaa.
 
Kutana na mama anayetumia ushirikina kumzuia mwanawe kumwoa msichana ampendaye kwenye bongo movie Prison Revenge, Jumatano saa 23:00 hapo Maisha Magic Bongo (151).
 
Mkude anasema kikundi cha sanaa walichokuwemo baadhi ya wasanii walianzisha hiyo na hata yeye Mkude akaambiwa analogwa na Sharo kupitia mafuta aliyokua anajipaka usoni Sharo Milionea kabla ya kulala.
 
Pamoja na hayo yote, Mkude Simba ambaye sasa hivi ana movie mpya ya Shobo Dundo sokoni anasema hakuvunja urafiki wake na Sharo na ndio maana alikua nae mpaka mwisho.
 
Amekiri pia ilibaki nusu aamini kwamba kweli Sharo analoga kupitia hayo mafuta ya kujipaka usoni maana ilikua kila siku kabla ya kulala lazima afanye hivyo baada ya kuosha uso, Marehemu mwenyewe alikua anasema ni kumsaidia uso kuwa na ngozi nzuri zaidi.
 
Mbali na kuitazama bongo movie kwenye Maisha Magic Bongo, pia unaweza kukodisha filamu kama Knock Knock kwenye BoxOffice kwenye DStv Explora yako. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:
 
Fill out my online form.