Producer wa Tanzania Nahreel

Producer wa Tanzania Nahreel kakataa kumpa beat staa wa hip hop

Producer maarufu wa Tanzania kwenye muziki wa bongofleva Nahreel ameingia kwenye top stories za leo kwenye DStv.com baada ya kukataa kumpa beat yake staa mmoja wa hip hop nchini Kenya.

Nahreel ambaye mikono yake ina hits tano kwenye nyimbo 20 za Clouds FM Top 20 ameweka wazi kuwa alimkatalia kurekodi baada ya kugundua kwamba jamaa hakuwa na pesa.
 
Kutana na wasanii waliofanya kazi na Nahreel kama Diamond Platnumz na Vanessa Mdee kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
"Jamaa alikuja studio, sitaki kumtaja jina ila aliniambia bwana inabidi tufanye kazi pamoja, tutengeneze wimbo... mi nikakubali na kazi ikaanza ila baada ya kumaliza kusuka kila kitu mwishoni akasema hana pesa ya kulipia beat, nikamkatalia."
 
Nahreel aliongezea, "Alijua sababu yeye analo jina kubwa labda ningempa beat for free ila ukweli ni kwamba sina hiyo, mimi nafanya biashara.... kila msanii unayemsikia juu ya beat ya Nahreel ujue amelipia, akaniambia basi naomba beat niende nayo nitakutumia pesa nikamwambia hapana, sifanyagi hivyo, tafuta pesa njoo lipia nitakutunzia beat yako."
 
Bei moja ya Nahreel inapatikana kuanzia shilingi milioni moja mpaka milioni moja na nusu za Kitanzania na mara nyingi Nahreel anapenda kufanya kila kitu kwenye studio yake, yani hapendi wala hataki kuuza beat peke yake, anapenda asimamie kazi beat yake itendewe haki na msanii hata kama ameiuza.
 
Kwa kweli usikose kuburudika na muziki kutoka East Africa kwenye Mzooka na vipindi vingine vipya kwenye Maisha Magic Bongo kama Mchichiko wa Pwani kila Jumatano saa 19:00 EAT. Haya yote unaweza kurekodi, kuchezesha tena (rewind) na pia kusimamisha wakati wowote (pause) kwenye DStv Explora yako. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:
 
Fill out my online form.