Msanii wa hit Amarula Roberto

Msanii wa Zambia mwenye hit single Amarula anakuja Tanzania siku ya Jumamosi 3 October.

Tarehe 3 October watanzania kwenye jiji la Mwanza watakutanishwa na mkali wa hit single ya Amarula, mwimbaji Roberto kutoka Zambia.

Roberto amethibitisha kuja Tanzania kwa ajili ya hii show ambayo itafanyika Jembe Beach Mwanza ikiwa imeandaliwa na Groove Entertainment pamoja na Jeme ni Jembe.
 
Hii itakua mara ya kwanza kwa mkali huyu kuja kuperform Tanzania ambapo amejulikana kutokana na single yake moja tu ya 'Amarula'
 
Pia burudika na single zingine kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz na King Kiba zitakazochezwa kwenye kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye channel mpya ya Maisha Magic Bongo (Channel 160).
 
Roberto alithibitisha kuja kwake kwa kuandika kwenye Twitter kwamba 'Tanzania mjiweke tayari'
 
Anasema wakati anarekodi Amarula hakujua kama ingekua kubwa na kupenya kwa kiasi hiki, ilikua ni idea tu ya kumsifia msichana na wala sio kinywaji kama mwanzoni ilivyodhaniwa.
 
Amarula imekua miongoni mwa hit singles ambazo zipo kwenye Top 10 zaidi ya tano za radio kubwa nchini Tanzania kwa zaidi ya wiki tano sasa hivi.