Mwigizaji wa Tanzania Richie Richie

Richie kaongea baada ya kushinda tuzo la AMVCA Nigeria

"Hatimaye tumepata ushindi... imani yangu kabla ilikua ni kushinda au kushindwa na nilikua tayari kwa chochote." Hayo ni maneno ya kwanza ya mwigizaji Richie Richie baada ya kutua uwanja wa ndege Dar es Salaam akitokea Nigeria baada ya kushinda kwenye AMVCAs 2016.

Mengi kuhusu Richie, Elizabeth Michael na waigizaji wengine kutoka bongo, usikose kuitazama Inside Bongowood, Jumanne saa 21:30 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Richie amesema, "Nigeria wamejipanga lakini ni watu ambao tukikaza tunaweza kuwashinda. Vile vile, nimejifunza mengi...sio kama tulivyokuwa tukifikiria, tukijipanga tunawakuta."
 
Kingine kikubwa alichosema mwigizaji huyu mshindi wa tuzo la Best Indigenous Language Movie (Swahili) kupitia movie yake ya Kitendawili ni kwamba Tanzania inabidi watu waanza kununua movie za kibongo kwa kasi.
 
"Ukiangalia tuna watu milioni 50 lakini mwigizaji akiuza movie yake mauzo hayafiki hata kopi milioni mbili, inahuzunisha... inabidi watu wasupport zaidi."
 
Waigizaji wa Tanzania Lulu (Elizabeth Michael) na Richie Richie walishinda tuzo mbili kwenye usiku wa tuzo hizi 5 March 2016 Lagos Nigeria, ambapo Lulu alishinda ya Best Movie Afrika Mashariki kwa movie yake Mapenzi.
 
Filamu hizi kutoka bongowood unaweza kuzitazama kwenye Maisha Magic Bongo. Pia unaweza kutazama zingine zaidi kupitia Catch Up Plus kwenye DStv Explora yako. Jaza fomu hii kupata Explora na pia Zapper decoder kwa urahisi: