Rich Mavoko star wa bongofleva kutokea WCB Wasafi ni msanii anaefanya vizuri sasahivi na nyimbo zake kuhit haswa mdundo wake wa sasahivi Kokoro.

Baada tetesi kuwa Muziki ya Darassa kudaiwa kufanya vizuri sasahivi na kufunika nyimbo nyingine zilizotoka nazo hivi karibuni na 'Kokoro' kutajwa kuwa kwenye list hiyo.
 
Kwa burudani zaidi, ungana na Rich Mavoko kupitia kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Rich Mavoko amefunguka kuhusu ya hili na kuyasema haya: “Zote hits kwa mpango wake na kila mtu na kila mtu anafanya kitu chake.” 
 
Mavoko amedai kuwa hata kabla wimbo huo haujatoka aliusikia na hata producer aliyeufanya ni mdogo wake, Abbah. Msanii huyo wa WCB pia amemsifia Darassa kwa kuweza kubadilika na kutoa hit single hiyo.
 
Mavoko alimaliza hivi, “Kuhusu masuala ya kuitrend YouTube, hizo ni habari za mtaani, unaweza ukagombana na mtu kwa vitu vingine vya kitoto.”