Msanii Rich Mavoko kutoka Tanzania

Rich Mavoko aelezea maisha ndani ya WCB

Ikiwa ni miezi tisa toka mkali wa hit ya Kokoro Rich Mavoko asaini WCB, amefunguka na kueleza maisha yake ndani ya label hiyo ya Diamond Platnumz.
 
Burudika na Kokoro ya Rich Mavoko kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
Nimeinasa hii ambapo  Rich Mavoko amedai maisha ya WCB ni mazuri na anaishi na wasanii wenzake kwa upendo na kushirikiano japmigongano haiwezi kukosekana kwa sababu za kibinadamu. 

Rich ameyasema haya, “Kusema kweli maisha ni mazuri sana, tunaishi kwa upendo, tunashirikiana, ni sehemu ambayo unaweza ukakaa na kufanya muziki nzuri kwa sababu watu ambao wanakuzunguka ni wasanii hata mabosi wetu, Sallam na Tale ni watu ambao wako kwenye huu muziki wa muda mrefu.” 

Aliongeza kuwa kwa upande wa muziki wake mpaka sasa ameona mafanikio makubwa hasa hasa kimataifa zaidi kwa kuwa nyimbo zake nyingi zinachezwa kimatifa.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kolabo zake za kimataifa.

Rayvanny pia ni msanii mwingine chini ya WCB na amesema haya kuhusu msanii angependa kufanya naye collabo.