BoxOffice

Account moja ya BoxOffice, watu wengi wa kukodisha filamu

BoxOffice yakuletea filamu moto kama Fast and Furious 7 na Get Hard, ambazo unaweza kukodisha na kutazama ukitulia sebuleni mwako wakati wowote.

Lakini itakuaje kama haupo nyumbani na kuna mtu anatamani akodishe filamu kwenye BoxOffice?

Usiwe na shaka, warahisishie kazi kwa kuongeza namba zao kwenye akaunti yako ya BoxOffice, ili pia wao waweze kukodisha filamu yoyote wanayotaka.

Cha kufanya, kwa kutumia simu yako ya mkononi, weka nambari ya simu ya unayemuongeza, nambari ya Smartcard ya dekoda yako, kisha tuma ujumbe huo kwenda namba 15111.

Uzuri ni kwamba, unaweza kuongeza namba za simu za watu watatu, ziwe nne pamoja na yako. Kwa namba zote nne mtaweza kukodisha filamu wakati wowote bila kikwazo.

Ni wewe utakayechagua ni akina nani utawaongeza kwenye account yako, iwe rafiki yako, mchumba hata mpangaji mwenzio ambaye anaitumia Explora yako.

Unaona ilivyo rahisi?

Na hata pale utapotaka kukodisha ila hauna pesa kwenye akaunti, wale uliowaongeza wanaweza kodisha ili mburudike na filamu hiyo pamoja. Ni Sh.5, 200 kwa kila filamu. Burudani kwenye BoxOffice kamwe haziwezi sitishwa!

Shirikisha jamaa zako wapate uhondo wa filamu moto moto, kwa kuongeza namba zao kwenye akaunti yako ya BoxOffice.

 

Related