DStv eazy self service

Twakuonyesha jinsi ya kulipa akaunti yako ya DStv kwa njia rahisi.

Kuwa karibu na akaunti yako ya DStv kwa kupitia simu yako ya mkononi, lipia malipo ya kifurushi chako cha mwezi, ingia M-Pesa, TigoPesa, EazyPesa, Airtel Money, FNB Bank mobile, NMB mobile au tembelea kibanda cha Selcom au Maxmalipo jirani kulipia.

Rudisha huduma yako endapo unakutana na ujumbe runingani, bonyeza *150*46# au ingia http://eazy.dstv.com, chagua namba za mwanzo zilizoambatana na ujumbe kwenye runinga, mfano E-16, E32, E18 na kubali kuondoa kisha huduma yako itarudi papo hapo.

Ziada, kwa kubonyeza *150*46# au kuingia http://eazy.dstv.com itakuwezesha kufahamu kiasi cha malipo unachohitaji kulipia, utaweza fahamu ni lini unahitaji kulipia na utaweza kuona kiasi cha pesa kilichobaki kwenye akaunti yako.

Pia utaweza kuhakiki na kurekebisha mawasiliano yako hapo, Mfano nambari yako ya simu ya mkononi au nyumbani, Barua pepe au eneo unaloishi. Ni huduma rahisi sana kwa mteja kutumia, anza sasa kuwa karibu na akaunti yako ya DStv.

Related