Artwork for the DStv Compact campaign

Tumewasikia, tunawajali. 

Sasa DStv inawaletea wateja wa kifurushi cha Compact matukio bora kabisa ya soka ulimwenguni bila gharama za ziada au ongezeko la bei ili kuwashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono.

Ligi bora za soka ulimwenguni, Ligi Kuu Ya Uingereza (the Barclays Premier League), Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), pamoja na Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) zitapatikana katika kifurushi cha Compact bila gharama ya ziada! Ofa hii kabambe itakuwa inapatikana katika chaneli mbili mpya za michezo, SuperSport 11 na SuperSport 12.