Msanii Raymond Rayvanny

Msanii Rayvanny amefunguka kuhusu msanii anaemkubali kutoka Tanzania na angetamanai sana kufanya nae collabo. Si mwingine bali ni Joh Makini kutoka kundi la Weusi.

Rapper A.Y naye ameongea haya kuhusu collabo yake na Joh Makini. Soma hapa.

“Bongo kuna wasanii wengi ambao ningependa kufanya nao kolabo lakini ukisema nimseme mmoja ambaye nawish ningefanya naye kitu ni Joh Makini,” alisema Rayvanny.
 
Burudika na hit ya Rayvanny Natafuta Kiki kwenye Mziki Fresh Jumatano saa 18:00 ndani ya Trace Mziki (323).
 
 “Joh namkubali sana na naona kama kuna kitu fulani cha ajabu kitatokea nikifanya naye kolabo. Bado sijamwambia Joh Makini, lakini nadhani ukifika muda kila kitu kitafanyika. Kila kitu kitajulikana hapo lakini kama nikikutana naye nataka kufanya kitu tofauti sana,” alimalizia Rayvanny.