MultiChoice Tanzania celebrates 20 years anniversary

Kampuni ya MultiChoice Tanzania inatimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania. MultiChoice inajivunia mafanikio yake katika soko la Tanzania toka kuanzishwa kwake mwaka 1997. Katika kipindi cha miaka 20, tumelihudumia soko la Tanzania kwa kutoa burudani za kiwango cha juu na ambazo hazipatikani sehemu yeyote ile.

Katika kipindi cha miaka 20 tumewaletea watanzania michuano ya mpira (World Cup, Euro Champions League, Europa League, EPL, La Liga, AFCON na makombe mengine mengi), pia tumeweza kuwaletea maudhui mengi kupitia chaneli yetu ya M-Net, Africa Magic na nyingine nyingi.

MultiChoice tumekua mstari wa mbele katika kukuza tasnia ya burudani nchini kwa kipindi chote cha miaka 20 wote mnakumbuka mchango wetu katika mziki kupitia Channel O, TRACE, MTV Base na sasa TRACE Mziki. Tasnia ya filamu tumechangia ukuaji wake kupitia Africa Magic na baadaye Maisha Magic East (channel 158) na sasa pia Maisha Magic Bongo (MMB) (channel 160) ambayo nimaalum kwa kazi za Kitanzania. Tumekuza michezo kupitia uwekezaji wetu kwenye riadha na michezo mingineyo.

Katika kusheherekea maadhimisho ya miaka 20, MultiChoice imeandaa maonesho ya siku mbili yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia siku ya Alhamisi tarehe 19 Oktoba na Ijumaa tarehe 20 Oktoba kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Katika maonesho haya utapata kushuhudia maendeleo ya teknolojia yetu ya tangu 1997 mpaka sasa na huduma mbali mbali zitolewazo na MultiChoice. Kutakuwa na mabanda kadhaa likiwemo la Supersport, M-Net, Maisha Magic Bongo, fashion, banda la watoto na mengine mengi.

Kutakua na ofa kabambe ndani ya siku mbili za maonesho, ambapo mteja atajipatia full set ya DStv kwa Tzs 59,000 tu, hii ikijumlisha kifurushi cha mwezi mmoja BURE kwa king’amuzi cha HD cha Zappa.

Kwa king’amuzi cha Explora mteja atapata full set kwa Tzs 240,000 pamoja na kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja BURE.

Ofa hii ni kwa siku za maonesho tu ambazo ni Alhamisi na Ijumaa hii tu. Hii si ya kukosa!

#20YearsOfAwesomeness!