MultiChoice Tanzania yatembelea Al Madina

Kituo cha watoto yatima cha Al - Madina kilianzishwa mwaka 2004 chini ya mlezi wao Mama Kuruthum Yusuf Juma ambaye aliguswa na wanawake wajane walioachwa na watoto wadogo  bila msaada wowote wa kujikimu kimaisha.

Kwa kipato kidogo alichokuwa nacho, Mama Kuruthum Yusuf alikusanya jumla ya watoto 7 na kuanza kuishi nao huko Tandika Azimio. Ilipofika mwaka 2006, walihamia makazi mapya, Tandale kwa Tumbo akiwa na jumla ya watoto 15 na ndipo walipo hadi hivi leo na idadi  ya watoto ikiwa imeongezeka na kufikia 57, ambapo  kati yao wasichana ni 23 na wavulana 34.

Mlezi huyu wa kituo, mama Kuruthum, ameelezea namna anavyolea watoto hawa katika mazingira magumu na kwa kipato kidogo ambacho kinapatikana kwa shida,  alisema “Tunategemea zaidi biashara ndogo ndogo ikiwemo ya kuuza maji kwa majirani kutoka kwenye kisima kilichopo hapa nyumbani kwetu, kushona nguo,  na misaada mbali mbali kutoka kwa majirani”.

MultiChoice Tanzania ilipata taarifa ya kituo hiki cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina mnamo mwaka 2009, na tumekuwa tukikitembelea kituo hiki kila mwaka na kuwapatia misaada midogo midogo kama vile vyakula, magodoro, majiko ya gesi, jokofu, mashuka, masufuria na vingine vingi

Vile vile imefunga king’amuzi cha DStv katika kituo hiki ili kuwapatia watoto pamoja na walezi wao burudani mbali mbali ikiwemo katuni  na vipindi vingine vyenye kuelielimisha na kuburudisha kama moja ya utaratibu wa kusaidia jamii.

Mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, MultiChoice ilikitembelea kituo na kufanya maongezi na mlezi wa kituo kuweza kufahamu maendeleo ya watoto kituoni hapa na kutaka kujua mahitaji yao ili tuone ni jinsi gani tunaweza kushiriana naye katika kuwalea watoto hawa.

 Bi Kuruthum alitupatia idadi ya vitu ambavyo vinahitajika kwa sasa.

Tunafurahi kusema kwamba, uwepo wetu hapa leo ni kuwakabidhi mahitaji yaliyotolewa na mlezi wa kituo kama ifuatavyo:

 

Mahitaji        

Idadi

Mikeka

6

Chupa za Chai

4

Sufuria 15kgs

3

Sufuria 10kgs

6

Beseni kubwa

3

Jagi

6

Tenga za Nguo

3

Shuka (4*6)

40

Godoro (3*6)

10

Godoro 4

1

Sahani

40

Vikombe

60

Kapeti (12*12)

12

Vyerehani

4