MultiChoice Tanzania

Msimu huu wa sikukuu, Multichoice Tanzania imetangaza neema kwa watanzania kwa kutoa ofa kabambe kwa wateja wake ambapo kuanzia tar 15 Novemba, mteja mpya wa DStv ataweza kuunganisha kwa shilingi 79,000 tu, hii kikiwa ni vifaa vyote pamoja na kifurushi cha DStv Bomba cha mwezi mzima.

Multichoice imekuwa na utamaduni wa miaka nenda rudi wa kuwapa zawadi wateja na watanzania kwa ujumla na kwamba kila ufikapo msimu kama huu, DStv huwatunuku wateja wake ili kuwawezesha kufurahia zaidi msimu huu wa sikukuu.

Tunafahamu kuwa msimu huu wa sikukuu familia nyingi zinaungana katika kusherehekea, hivyo DStv imeamua kuwaongezea burudani kwa kutoa ofa hii kabambe. Badala ya mteja mpya kulipa shilingi 98,000 kwa ajili ya kuunganishwa pamoja na kifurushi cha mwezi, sasa watalipa shilingi 79,000 tu na kuunganishwa na DStv pamoja na kifurushi cha Bomba cha mwezi mzima.

Tunapokuwa nyumbani na familia zetu, watoto wanataka waangalie katuni, kinamama tunapenda kuangalia vipindi kama vile vya mapishi, urembo, na tamthilia, kinababa nao hupenda sana kutazama michezo mbalimbali kama kandanda na kadhalika. Ni kwa msingi huu tumeamua kuwarahisishia burudani hii inayopatikana kutoka DStv.

Ofa hii ni kwa nchi nzima na itaendelea kwa miezi miwili hadi Januari 15, 2018.

Ofa hii kwa wateja wapya inakuja siku chache tu baada ya DStv kuanza kutoa zawadi kwa wateja wake kwa kuwaongezea chaneli za SuperSport kwenye vifurushi vyao punde walipiapo akaunti zao kabla hazijakatika.

Katika ofa hii ya kuongezewa channel, wateja wa kifurushi cha Compact na Compact Plus watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika kifurushi cha DStv Premium kwa kipindi cha siku saba mfululizo bureeee!

Hali kadhalika, watumiaji wa kifurushi DStv Bomba na DStv Family nao watapata chanel zote za Supersport zinazopatikana kwenye kifurushi DStv Compact na hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (Premier League) na mashindano mengine makubwa kwa siku saba mfululizo bureee!

Multichoice Tanzania imekuwa ikitoa huduma za DStv hapa nchini kwa Zaidi ya miaka 20 sasa na imeendelea kuwa kinara katika kuwapatia watanzania habari, elimu na zaidi ya yote burudani kabambe.